BEI ZA UKUMBI WA KENYATA

IDADI YA WATU BEI IDADI YA WATU BEI
100 – 150 2,500,000 450 5,500,000
200 3,000,000 600 7,000,000
250 3,500,000 700 7,500,000
300 4,000,000 800 8,000,000
350 4,500,000 900 8,500,000
400 5,000,000 1,000 9,000,000

NB:
UKUMBI WA MUGABE KWA WATU 200 NI TSH 3,500,000 NA KWA WATU 250 NI 4,000,000. GHARAMA ZA UKUMBI ZINAJUMUISHA HUDUMA ZIFUATAZO

  1. Viti na Meza kulingana na idadi ya watu
  2. Generator umeme ukikatika
  3. Watu wa usafi maliwatoni
  4. Stage na Red carpet ukumbini
  5. Kumbi za Mandela na Obama zinatolewa kwa idadi ya watu kuanzia 400 na kuendelea.
  6. Fridge ya kuwekea vinywaji ukumbini.
  7. Room moja ya kulala maharusi na kifungua kinywa asubuhi,ofa hii utapata ikiwa idadi yako ya watu ni kuanzia watu 200 na kuendelea.
  8. Eneo la kupaki magari na sio kulinda magari ( Park at your own risk)

VITU VIFUATAVYO VITACHAJIWA KAMA UTAHITAJI

Eneo la kupikia 200,000/= ( Ni eneo tu na sio jiko wala vyombo)

Wapambaji wanapaswa kulipia 200,000/= kabla ya kuanza kupamba au kuingiza vitu vyao.Gharama hizi ni kwa sababu ya uharibifu mdogo mdogo na uchafu wanaoucha ukumbini.Mwenye sherehe mueleze mpambaji wako mapema kuhusiana na gharama hizi za 200,000/=

Eneo la kuchinjia ndafu ni Tsh 25,000/= kwa kila ndafu

MASHARTI YETU NI

  • Unatakiwa kulipa 50% ya jumla ya hela ya sherehe kwa ajili ya kushikilia ukumbi wako na kabla ya siku 5 ya sherehe kuanza uwe umekamilisha malipo yote.
  • Haturuhusu shughuli za upambaji kuanza kabla malipo hayajakamilika.
  • Haturuhusu chakula kuingia ukumbini kikiwa kwenye sufuria au ndoo za rangi, Chakula kiwekwe kwenye Hot pot au ndoo nyeupe.
  • Wapishi na wahudumu wawe wamevaa uniform safi na nzuri; masharti haya yasipofatwa chakula hakita ruhusiwa kuingia ukumbini;
  • Haturuhusu kuchinja ng’ombe katika eneo la hotel.
  • Vinywaji vije siku/tarehe husika ya sherehe.
  • Tarumbeta haziruhusiwi mwisho wa tarumbeta ni getini. Na pikipiki(Toyo) haziruhusiwi kuingia hotelini.
  • Baada ya sherehe kuisha wahusika wanaombwa kuchukua vitu vyao kama crets,decorations etc
  • Ongezeko la watu kwa kila kiti litachajiwa Tsh 10,000
  • Pesa ikishalipwa hairudishwi.
  • Haturuhusu mifuko ya plastic eneo la hotelini.
  • Wapambaji wanapaswa kuondoa uchafu baada ya kumaliza kazi yao.Mfano majani waliotumia kupambia,Maua etc
  • Wapambaji hawaruhusiwi kutoboa ukuta wala kuweka sticker kwenye tiles.Wala kufanya shughuli za kugonga gonga ukumbini.
  • HAKUNA PUNGUZO LA BEI.   
  • MWISHO WA SHEREHE KUMALIZIKA NI SAA SITA KAMILI USIKU.

ASANTE NA KARIBU TUKUHUDUMIE

Photos